“Imamu 12 Baada ya Mtume saww”

HADITH YA 12 IMAMS BAADA YA MTUME saww

Jabir ibn Samura amesimulia: Nilimsikia Mtume (saww) akisema: “Kutakuwa na Maimamu kumi na wawili.” Kisha akatamka sentensi ambayo sikuweza kuisikia. Baba yangu akasema, Mtume aliongeza, “Na wote watatokana na Maquraysh.”
[Sahih al-Bukhari ( Ya Kiingereza), Hadithi namba 9.329, Kitabul Ahkam; Sahih al-Bukhari, (Ya Kiarabu), 4:165, Kitabul Ahkam]
Mtume (saww) akasema: “Dini (Uislamu) itaendelea mpaka Saa (ya Kiyama), na kuwepo kwa Maimamu kumi na wawili kwa ajili yenu, wote watatokana na Maquraysh.”
[Sahih Muslim, (Ya Kiingereza), Sura ya 754, juzuu ya 3, uk1010, Hadith namba 4,483, Sahih Muslim (Ya Kiarabu), Kitab al-Imaara, 1980 Toleo la Saudi Arabia, Juzuu ya 3, Uk 1453, Hadith namba 10

WRITTEN BY: Taahir

No comments yet.

Leave a reply

Reset all fields